Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) inashiriki Maonesho ya “World Travel Market London 2024”
ambayo yanafanyika katika jiji la London, Uingereza kuanzia tarehe 5- 7
Novemba, 2024.
Maonesho hayo ambayo taasisi
mbalimbali za Wizara ya Maliasili na Utalii zinashiriki, NCAA inatumia fursa
hiyo kunadi vivutio vya utalii ikijumuisha uzuri wa asili wa Ngorongoro,
wanyamapori wa aina mbalimbali wakiwepo 'Big 5', vivutio vya urithi wa utamaduni
na mambokale vilivyopo eneo la Ngorongoro ambalo ni Urithi wa Dunia
linalotambuliwa na UNESCO.
Mwaka 2023 eneo la Hifadhi ya
Ngorongoro lilitangazwa kuwa kivutio bora cha utalii barani afrika ambapo eneo
hilo ni moja ya maajabu 7 barani afrika na eneo la kipekee lenye hadhi tatu
(03) za kimataifa zinatotambuliwa na UNESCO ambazo ni Urithi wa Dunia
mchanganyiko (asili na utamaduni), Biosphere Reserve na UNESCO Global Geopark
inayohusisha utalii wa miamba.
Aidha, kwa mujibu wa mtandao wa tripAdvisor kwa
takribani miaka mitatu mfululizo iliyopita eneo la Ngorongoro lilichaguliwa
kama eneo bora kwa watalii waliotembelea (best of the best) kwa wageni wa
mataifa mbalimbali wanaotembelea kwa
nyakati tofauti.
Ujumbe wa NCAA umeongozwa na Kamishna
wa Uhifadhi Dkt. Elirehema Doriye ambapo katika maonesho hayo wanakutana na
mawakala wa utalii na wadau mbalimbali kwa ajili ya kunadi vivutio vya utalii
na fursa za uwekezaji zilizopo hifadhi ya Ngorongoro, Soko la Uingereza na
mataifa ya ulaya ni moja ya maeneo ya kimkakati wenye wageni wengi
wanaotembelea nchi yetu.
0 Maoni