Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff
amemtaka Mkandarasi MAC Contractor Ltd anayejenga Daraja la Mohoro lililopo
Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani
kukamilisha ujenzi wa nguzo mbili zilizobakia
kwenye ujenzi wa daraja hilo
kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Mhandisi
Seff ametoa agizo hilo ikiwa ni siku tatu tangu kupita eneo hilo la ujenzi na
leo kurudi tena ili kujionea hatua ya kuangalia maagizo yake ya awali
aliyoyatoa kama yametekelezwa.
Aidha, Mhandisi
Seff, amemtaka Mhandisi Mshauri wa TREECO Mhandisi Emmanuel Mahimbo kumsimamia
Mkandarasi MAC ili amalize kazi kwa wakati.
Katika hatua
nyingine Mhandisi Seff ametembelea tena mradi wa ujenzi wa barabara ya
Utete-Kingupira (Km. 32) inayojengwa kwa kiwango cha changarawe kwa kutumia
Teknolojia Mbadala ya ECOROADS na Mkandarasi NRST LIMITED CIVIL WORKS
CONTRACTOR JV DASHAS COMPANY LIMITED.
Mhandisi
Seff hakuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumuelekeza Kaimu
Meneja wa TARURA Wilaya ya Rufiji Mhandisi Nicolaus Ludigery kuhakikisha
Mkandarasi NRST anawasilisha mpango kazi wake unaoonyesha namna atakavyofidia
siku zilizopotea na kukamilisha kazi kwa wakati, vinginevyo hatua za kimkataba
zitachukuliwa.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Utete-Kingupira
umepangwa kukamilika mwezi Aprili 2025.


0 Maoni