Katibu Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, anatarajiwa
kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za CCM Mkoa wa Mwanza tarehe
20 Novemba 2024, akiongoza viongozi na makada wa CCM waliotumwa maeneo
mbalimbali nchini kwa kazi hiyo.
Balozi
Nchimbi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, atazindua kampeni hizo
katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Furahisha, Nyamagana, jijini
Mwanza.
Wajumbe wa
Kamati Kuu ya CCM, ambao ni walezi wa mikoa mingine, pamoja na Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wamepewa jukumu la kuzindua kampeni hizo
katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa tarehe hiyo hiyo.
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, atazindua kampeni Mkoa wa Mbeya, huku
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Mohamed Dimwa, akizindua
kampeni Mkoa wa Katavi.
Viongozi
wengine wa CCM waliopangiwa kuzindua kampeni ni pamoja na:
- *Ndugu
Issa Haji Usi Gavu*, Katibu wa NEC - Oganaizesheni, mkoani Geita.
- *Ndugu
Amos Gabriel Makalla*, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, mkoani Dar
es Salaam.
- *Ndugu
Rabia Himid Abdalla*, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, mkoani
Kilimanjaro.
- *Mhe. Dkt.
Isdory Phillip Mpango*, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
mkoani Dodoma.
- *Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa*, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
mkoani Kigoma.
- *Mhe.
Hemed Abdulla Suleiman*, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, mkoani Tanga.
- *Mhe.
Zuber Ali Maulidi*, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mkoani
Singida.
Viongozi
wengine ni pamoja na:
- *Komredi
Mary Pius Chatanda*, Mwenyekiti wa UWT Taifa, mkoani Arusha.
- *Ndugu
Mizengo Kayanza Pinda*, Waziri Mkuu Mstaafu, mkoani Mtwara.
- *Ndugu
Halima Mamuya*, mkoani Njombe.
- *Ndugu
Nasir Ally Juma*, mkoani Tabora.
- *Ndugu
Mohamed Aboud Mohamed*, mkoani Iringa.
- *Komredi
Mohamed Ali Mohamed Kawaida*, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, mkoani Morogoro.
- *Ndugu
Fadhili Maganya*, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, mkoani Simiyu.
- *Dkt.
Dotto Mashaka Biteko*, Naibu Waziri Mkuu, mkoani Mara.
- *Ndugu
Hussen Bashe*, mkoani Shinyanga.
- *Ndugu
Livingstone Lusinde*, mkoani Manyara.
- *Ndugu
Ally Hapi*, mkoani Kagera.
- *Ndugu
Nape Nnauye*, mkoani Rukwa.
- *Ndugu
Zainab Shomari*, mkoani Lindi.
- *Ndugu
Salim Faraji Abri (Asasi)*, mkoani Ruvuma.
- *Ndugu Jokate
Mwengelo*, mkoani Pwani.
- *Richard
Kasesela**, Mjumbe wa NEC, mkoani Songwe.
Mkakati huu
wa kuzindua kampeni kwa mtindo wa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi wakuu
na wanachama unaonesha jinsi CCM inavyothamini uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia, unadhihirisha dhamira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vya
upinzani, ambavyo hadi sasa vimeshindwa kusimamisha wagombea wa kutosha
kushindana kikamilifu.

0 Maoni