Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya chama hicho Ijumaa, Novemba 29, 2024 kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, uliofanyika jana Novemba 27, 2024.
Taarifa ya kikao hicho iliyotolewa leo Novemba 28, 2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, imeeleza kuwa kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Mrema amesema kikao hicho kitajadili agenda kuu moja ya yaliyojiri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na kuongeza kuwa kauli ya chama itatolewa baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
0 Maoni