Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekuwa mtu wa
kwanza kununua hati fungani za Samia Infrastructure Bond, ambapo amenunua hati fungani
zenye thamani ya shilingi milioni 100.
Dkt. Mpango
amenunua hati fungani hizo leo akizindua rasmi Samia Infrastructure Bond, ambayo
ni ushirikiano wa CRDB Bank na TARURA ikiwa na lengo la kuwezesha wakandarasi
wazawa wanaotekeleza miradi ya miundombinu iliyoanzishwa kwa chini ya TARURA.
Makamu wa
Rais Dkt. Mpango ametoa wito kwa wananchi, vikundi na taasisi kuwekeza kwenye
hatifungani ya Samia Infrastructure Bond iliyozinduliwa leo, ikiwa na lengo la
kuwezesha wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi iliyo chini ya TARURA.
Katika
hotuba yake Dkt. Mpangoa ametaka kutolewa wa elimu ya masuala ya fedha na
uwekezaji wakati akizindua Samia Infrastructure Bond iliyoanzishwa kwa
ushirikiano kati ya CRDB Bank na TARURA.
0 Maoni