CCM yashtushwa kuuawa Katibu Mkuu CCM wilaya ya Kilolo

 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi. Christina Kibikia liyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla imesema kuwa marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria Semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.

CPA Makalla amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM mkoa wa Iringa kufuatia kifo hicho cha ghafla na cha kikatili.

Amemalizia kwa kusema kuwa, “Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.”

Chapisha Maoni

0 Maoni