Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), Mhe.
Kapt. George Mkuchika Oktoba 28, 2024 amewasha umeme katika Kijiji cha Magenge
kilichopo kwenye Tarafa ya Nongwe wilayani Gairo mkoani Morogoro, Kijiji hicho
ni kati ya vijiji nane vilivyokuwa vimesalia kupata umeme kwenye tarafa hiyo
ambapo kwa sasa vyote nane tayari vimepata umeme na vipo tayari kuwashwa.
Pia amekagua ujenzi wa daraja la Lebenya ambalo linagharimu
zaidi ya shilingi milioni 300 ambapo ujenzi huo ukikamilika utanufaisha kata
saba zenye jumla ya wakazi 766,507 na kurahisisha kusafirisha mazao ya wakazi
wanaoishi katika wilaya za Kilosa, Gairo na Kilindi.
Aidha, amezindua Kituo cha Afya Iyogwe kilichopo katika Kijiji cha Iyogwe wilayani humo ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 500 ambacho kinahusisha jengo la wazazi na upasuaji, maabara, nyumba ya mtumishi na jengo la kuhifadhi maiti.
0 Maoni