Waziri Chana akutana na Machifu na Wazee wa kimila wa eneo la Lyamba Lyamfipa

  

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Machifu kutoka Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa kwa lengo la kujadiliana namna ya kuwa na uhifadhi endelevu wa eneo hilo la misitu.

Kikao hicho kimefanyika jana Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza machifu hao kwa juhudi zao za kuhifadhi eneo hilo muhimu kwa Taifa katika utunzaji wa mazingira.

Hifadhi ya Misitu ya Miteremko ya Safu za Milima ya Lyamba Lyamfipa ina vyanzo vingi vya maji ambayo yanatumiwa na wananchi kwa matumizi ya nyumbani na kwenye kilimo cha umwagiliaji na pia ndio chanzo cha mvua kwa eneo la Sumbawanga.



Chapisha Maoni

0 Maoni