Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally
Possi akizungumza na wajumbe wa kikao kazi cha kuandaa Kanuni za Urejeshaji wa
Gharama za Uendeshaji wa Mashauri ya Serikali wakati akifungua kikao hicho
kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Msaidizi Udhibiti Ubora wa
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Mercy Kyamba akizungumza na wajumbe wa
kikao kazi wakati akimkaribisha Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi
kufungua kikao hicho cha kuandaa Kanuni za Urejeshaji wa Gharama za Uendeshaji
wa Mashauri ya Serikali kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mwandishi Mkuu wa Sheria Msaidizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Nicodemas Chuwa akiwasilisha mada kuhusu Uandishi wa Sheria Ndogo wakati wa kikao kazi cha kuandaa Kanuni za Urejeshaji wa Gharama za Uendeshaji wa Mashauri ya Serikali kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha kuandaa Kanuni za Urejeshaji wa Gharama za Uendeshaji wa Mashauri ya Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufungua kikao kazi cha kuandaa Kanuni za Urejeshaji wa Gharama za Uendeshaji wa Mashauri ya Serikali kilichofanyika Kibaha mkoani Pwani.
0 Maoni