Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 14, 2024 ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbulizi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mt. Francis Xavier Nyakahoja.
Katika Ibada hiyo Viongozi mbalimbali
wa Kitaifa wamehudhuria akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi,
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Doto Biteko, Jijini Mwanza.
0 Maoni