Nchi ya Marekani imetoa tahadhari ya hali
ya usalama kwa raia wake waishio nchini Msumbiji hususan waliopo katika mji
mkuu wa Maputo.
Tahadhari hiyo inafuatia kuongezeka
kwa maandamano katika maeneo mbalimbali mjini Maputo, kwenye barabara
zinazoelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, na katika miji mingi kote
Msumbiji.
Ubalozi wa Marekani mjini Maputo
umewataka raia wake waishio nchi hiyo kufahamu hali hiyo ya dharura.
Hapo jana tume ya uchaguzi ilitangaza
kwamba chama tawala cha Msumbiji, Frelimo, kimeshinda uchaguzi huo uliogubikwa
na malalamiko na kuligawa taifa hilo.
0 Maoni