Kampeni ya ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi yaendelea

 

Wananchi na viongozi wa jimbo la Musoma Vijijini wanashirikiana na Serikali kuharakisha ujenzi wa maabara tatu kwenye kila Sekondari ya Kata.

Ujenzi wa maabara hizo unaendelea na Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo anaendelea kupiga Harambee ili kukamilisha ujenzi huo.

Taarifa iliyotolewa na mbunge wa Musoma Vijijini inaeleza kuwa Sekondari ambazo hazina maabara ni pamoja na za Bukwaya, Busambara, Mtiro, Murangi, Nyanja, Seka na Tegeruka.

Jimbo hilo pia linasekondari nne ambazo zina maabara moja ambazo ni za Bukima, Dan Mapigano, Kasoma na Mabuimerafuru.

Wadau wa Maendeleo na hasa Wazaliwa wa Musoma Vijijini wanaombwa wajitokeze kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zetu za Kata, imesema taarifa hiyo.

Jimbo la Musoma Vijijini lina Sekondari za Kata/Serikali 26, Sekondari za Binafsi 2 pamoja na  Sekondari mpya zinazojengwa 12.

Kwa sasa jimbo hilo lenye maabara 41 za Masomo ya Sayansi (physics, chemistry & biology) kwenye Sekondari za Kata, linauhitaji wa maabara 78.

Chapisha Maoni

0 Maoni