Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mfalme wa Lesotho Mfalme Letsie III katika Ikulu ya Kifalme iliyopo Maseru nchini humo. Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Lesotho.
Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Lesotho na Miaka 200 ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Lesotho zitakazofanyika katika Uwanja wa Setsoto Mjini Maseru.
0 Maoni