Barcelona yaishushia kipigo Real Madrid

 

Robert Lewandowski ametupia wavuni magoli mawili ndani ya dakika tatu nakuisaidia Barcelona kuichakaza Real Madrid kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga.

Real Madrid ambayo ilikuwa ikitafuta rekodi ya kucheza michezo 43 bila ya kufungwa inayoshikiliwa na Barcelona ilijikuta ikitibuliwa mahesabu yao katika kipindi cha pili.

Robert Lewandowski alifungua karamu ya magoli dakika ya 54 na kisha kutumbukiza goli la pili dakika datu baadae, huku magoli mengine ya Barcelona yakiwekwa kimiani na Lamine Yamal na Raphinha.

Katika mchezo huo Lewandowski alikosa nafasi mbili za kuweza kufunga hat-trick. Kwa ushindi huo Barcelona wanaongoza ligi ya La Liga kwa tofauti ya pointi sita.

Chapisha Maoni

0 Maoni