Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na ujumbe wake akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya
Benki ya Citibank ya Marekani , Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki
hiyo, jijini New York, Marekani. Septemba 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na ujumbe wake akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya
Benki ya Citibank ya Marekani , Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki
hiyo, jijini New York, Marekani. Septemba 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Citibank ya
Marekani, Bw. John Dugan, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye makao
makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani. Septemba 24, 2024. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya
Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha
kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT).
Amesema hayo
jana (Jumanne, Septemba 24, 2024) mara baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Bodi
ya Benki hiyo, Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New
York, Marekani.
“Serikali ya
Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi
wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik
amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,”
alisema.
“Benki hii
imekuwa ikikopesha makampuni yanayojenga reli yetu ya SGR na ili kuhakikisha
wanachangia ujenzi wa uchumi wa Tanzania, na wao pia wamechukua lot moja ya
ujenzi wa reli hiyo na kufadhili ujenzi wake. Hali kadhalika uendelezaji wa
uwanja wa ndege wa Pemba.”
Alisema
Tanzania ilipokabiliwa na uhaba wa mafuta ya kuendeshea mitambo na magari,
benki hiyo ilitumika kuwasaidia wafanyabiashara kupata mafuta kwa bei nafuu,”
alisema.
Mbali na
ushauri wa masuala ya kiuchumi, Waziri Mkuu amesema benki hiyo kwa kushirikiana
na taasisi ya kimataifa ya maendeleo ya Marekani, (U.S. International
Development Finance Corporation) pia ilitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo
huku ikiwapatia fursa zaidi akina mama na wadada wanaomiliki biashara zao
binafsi.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Citibank ya Marekani, Bw. John Dugan
amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ya
kimaendeleo kama walivyofanya katika mika 40 iliyopita.
0 Maoni