Mafuriko yaua na kusababisha maafa nchi za Ulaya

 

Watoa huduma za dharura wanakabiliana na athari za mafuriko eneo la Kati na Mashariki mwa Ulaya kufuatia mvua ya kimbunga Boris iliyosababisha mito kufurika na kuharibu maelfu ya nyumba.

Mtu mmoja ameripotiwa kufa nchini Poland, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Donal Tusk amethibitisha leo Jumapili.

Kimbunga Boris kimesababisha maafa pia Romania Jumamosi, ambapo watu wanne wamekufa kutokana na mafuriko kusini mashariki mwa mkoa wa Galati.



Chapisha Maoni

0 Maoni