Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze
mkoani Pwani amepokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Msoga na
madawati 120 kwa ajili ya shule za msingi mbili za Chalinze.
"Kwa
mujibu wa takwimu za makusanyo na mapato, NMB- Chalinze ndiyo tawi namba moja
Tanzania kwahiyo maana yake NMB wanapozungumza tunapata Bilioni 500 ni pamoja
na mchango mkubwa wa Chalinze," alisema Kikwete wakati akipokea vifaa
hivyo.
Kikwete
amezishauri zaidi sekta binafsi nyingine nyingi kushirikiana na serikali katika
kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ili kuwa na uchumi endelevu na
kurudisha kwa wananchi ambao ndiyo wateja wakuu.
Tukio hilo
muhimu la ustawi wa wananchi limefanyika mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Mhe. Shaibu Ndemanga, Mkurugenzi wa Halmashauri Ramadhani Possi, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Chalinze Mhe. Hassani Mwinyikondo huku benki ya NMB iliyotoa
msaada huo ikiongozwa na Mkuu wa Idara ya Mitandao ya Matawi na Mauzo ya NMB
Ndugu Renatus Richard.
0 Maoni