JKCI kuendesha kambi ya moyo Septemba 28 na 29

 

Katika kuadhimisha Siku ya Moyo Duniani tarehe 29/9/2024 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika bila malipo yoyote yale kwa watoto na watu wazima tarehe 28-29/09/2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakata Kikwete (JKCI) iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya Tuari.

JKCI imewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili kujua kama wana matatizo ya moyo ili kuanza matinanu mapeka kwa anayegundulika kuwa ni mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasisliana kwa simu namna 0754578190, 07839225571 na 0674179036 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.

Chapisha Maoni

0 Maoni