Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed
Mchengerwa amesema hakuna mgonjwa anayesafirishwa kwa njia ya Pikipiki huku
akiwa amewekwa kwenye Tenga kupelekwa kupata huduma za Afya.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati akitoa salaam za Ofisi ya Rais - TAMISEMI
kwenye mkutano wa hadhara wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa
Tunduru uliofanyika kwenye uwanja wa CCM wilayani jana.
Amesema
nimeona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha mgonjwa
akisafirishwa kwenye Pikipiki huku akiwa kwenye Tenga na kueleza kuwa hakuna
magari ya kusafirishia wagonjwa na kwa yaliyopo huwagharimu wananchi fedha
nyingi kwa ajili ya kupata huduma ya Gari la Wagonjwa.
Napenda
kukuthibitishia Mhe. Rais hapa Tunduru hakuna upungufu wa magari ya kubebea
wagonjwa na kati ya Magari 535 tuliyoyakabidhi mwaka jana kwa muongozo wako
Mhe. Rais hapa Tunduru walipata Magari 4 ya kubebea wagonjwa.
Na Magari
hayo yalipekwa kwenye Kituo cha Afya Nakapanya, Matemanga, Mtesi na Kituo cha
Afya Nyalasi ambayo yanafanya kazi saa 24 na rufaa zote zinaratibiwa kwa
utaratibu maalumu na sio kuchangisha wananchi.
‘Utaratibu
unaotumika kusafirisha wagonjwa nikutumia magari ya kubebea wagonjwa
(Ambulaces) na kwa kutumia madereva ngazi ya jamii waliosajiliwa wakati wa mfumo wa M-Mama ambapo mfumo huu unahusika na
kusafirisha wakina mama wajawazito na watoto wachanga bila malipo yoyote.
Aliongeza
kuwa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ina jumla ya madereva wa jamii 20
walioingia mikataba na Serikali; Hivyo taarifa hizi zipuuzwe kwani zinalengo la
kuupotosha umma, kuleta taharuki kwa jamii nakuichafua Serikali.
0 Maoni