Waziri Dkt. Kijaji atembelea Maonesho ya Nanenane

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo, Bi. Sarah Kibonde muda mfupi baada ya kuwasili katika Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024. Wa kwanza kulia ni Meneja wa NEMC Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Caren Kahambwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ashatu Kijaji akipata maelezo kutoka kwa Mtumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bi. Mariam Abtwaib wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali zilizoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi nan Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoka kwa Meneja wa NEMC Kanda ya Kati Dodoma Dkt. Caren Kahambwa katika Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma leo Alhamisi Agosti 8, 2024.


Chapisha Maoni

0 Maoni