Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu
Hassan amekabidhi cheti cha pongezi kwa ushiriki wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) kwenye tamasha la Kizimkazi Festival 2024 Hafla ya chakula
cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi Zanzibar.
Cheti hicho cha pongezi kimepokelewa kwa niaba ya Kamishna
wa Uhifadhi wa TANAPA, Nassoro Juma Kuji, na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,
Jully Bede Lyimo - Mkuu wa kitengo cha
Maendeleo ya Biashara pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi Amina R. Salum
ambaye ni Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Ruaha.
TANAPA, kwa dhati na unyenyekevu mkubwa tumepokea na kuthamini heshima hii kubwa kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

0 Maoni