Polisi yapiga marufuku vijana wa CHADEMA nchini kukusanyika Mbeya

 

Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina yoyote ile ya ndani au nje inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani kwani inalenga kuleta uvunjifu wa amani Mkoa wa Mbeya na maeneo mengine yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo mkoani Mbeya na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo CP Awadh J. Haji kufuatia kuwepo kwa mipango ya viongozi wa CHADEMA kuhamasisha vijana kote nchini kukusanyika Mkoa wa Mbeya Agosti 12, 2024 kwa lengo la kufanya maandamano na mikusanyiko kwa mwamvuli wa maadhimisho ya siku ya vijana duniani.

“Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii wameonekana na kusikika baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo [CHADEMA] wakihamasisha vijana kote nchini, viongozi wa kitaifa wa chama, kamati kuu ya chama hicho na kualika baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuadhimisha siku ya vijana mkoani Mbeya,”amesema CP Haji.

Amesema pamoja na mwaliko wanaotoa, viongozi hao wameendelea kutoa kauli ambazo hazionyeshi kuwa na lengo la kwenda kuadhimisha siku ya vijana duniani bali ni kwenda kuhamasisha kufanya vitendo vinavyolenga uvunjifu wa amani kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya.

Miongoni mwa kauli hizo ambazo zinaashiria kuwa na lengo la kuvuruga amani ni za Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa ndugu Twaha Mwaipaya, “Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo yatarehe 12/08/2024 tuna kwenda kuweka hatma yaTaifa letu la Tanzania mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanjawa Ruanda Nzovwe Mbeya” amenukuu CP Haji.

Kauli nyingine ni, “Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wa mejitambua, siku yatarehe 12/08/2024 tuna kwenda kuacha uteja kwa serikali vijana wakitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025.”

Amesema Jeshi la Polisi nchin ilinatoa onyo kali na katazo kwa mtu au kikundi cha watu kinachojipangak ufanya maandamano na mikusanyiko kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi lipo imara na limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi, usalama, amani na utulivu vinatawala nchini na lipotayari kuzuia na kupambana na viashiria vyovyote vya uvunjifu waamani, na halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibuwa sheria kwa mtu yeyote atakayekiuka katazo hili.

Chapisha Maoni

0 Maoni