Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kwela, Mhe. Deus Sangu
amewahakikishia  wananchi kuwa  atafanya kazi kwa weledi na uaminifu wa hali
ya juu  huku  akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa  aliyowapa 
wananchi wa Jimbo la Kwela na Mkoa wote wa Rukwa  kwa kumteua yeye  kuwa Naibu Waziri wa Ofisi yake.
Aidha, Mhe. Sangu amewashukuru wananchi wote  wa Mkoa wa Rukwa kwa mapokezi makubwa  waliyompa mara baada ya kuwasili Mkoani humo,
ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.
Mhe. Sangu  ametoa
kauli hiyo  kwa nyakati tofauti wakati
akizungumza na Watumishi pamoja na wananchi 
katika  Kata ya Kanda na  Kaengesha 
kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika 
kwenye Vijiji vitano  vya Jimbo la
Kwela , Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga 
Mkoani  Rukwa.
Amesema Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaheshimisha
wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kumteua yeye ili aweze kumusaidia kuwahudumia
Watanzania katika masuala ya utumishi na utawala bora.
"Naomba niwaahidi katika najukumu yangu haya mapya
nitakuwa mnyenyekevu, mchapakazi, mweledi na mwaminifu katika kutekeleza
majukumu yangu ya kumsaidia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene " amesema Mhe. Sangu.
Ameongeza "Nawashukuru pia wananchi wa Kwela kwa
kuniamini na kunituma Bungeni ili nikawesemee changamoto zinazowakabili hii
imepelekea Rais Samia kuweza kuniona na kuniteua kushika Wadhifa huu.
Katika hatua nyingine Mhe. Sangu ametumia fursa hiyo
kumshukuru Mhe.Rais kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo la
Kwela ikiwemo ujenzi wa zahanati, barabara, maji pamoja na umeme.
Mhe. Mhe. Sangu amewahakikishi wananchi hao kuwa  “Mambo mazuri zaidi yanakuja, Rais Samia
amesema anataka kuiona  Kwela   yenye nuru kiuchumi,” amesisitiza Mhe.Sangu.
Amesema Mhe.Rais anawapenda sana wananchi wake hususan wa
Mkoa wa Rukwa ndio maana ameongeza bei ya mazao ya mahindi   hadi Sh.700 kwa kilo moja ili kuhakikisha
wananchi wa Kwela wananufaika kiuchumi kupitia kilimo chao.
Hata hivyo Mhe.Sangu ameowaonya wananchi wake wasithubutu
kuuza mazao yote la sivyo kufikia Mwezi Januari mwakani watakumbwa na baa la
njaa.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Mhandisi, Daudi Sebiga ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mhe.Deus Sangu kwani Mchapakazi na Mwaminifu wa kiwango cha hali ya juu sana.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu akizungumza na Elus Homera mara baada ya kuwasili katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Kanda, ikiwa ni ziara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Kanda, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wakimshangilia kwa shwange Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deus Sangu mara baada ya kuwasili, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.



0 Maoni