Maandamano yamng’oa Waziri Mkuu Bangladesh, aikimbia nchi

 

Makundi ya watu waliojawa na furaha wamevamia mitaa mbalimbali nchini Bangladesh, kusherehekea kujiuzulu na kukimbia nchi Waziri Mkuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu Sheikh Hasina.

Watu wamekuwa wakipeperusha bendera ya taifa hilo na kucheza juu ya vifaru vilivyoegeshwa katika Jiji la Dhaka, Shirika la Habari la AFP imeripoti.

Kituo cha runinga cha Channel24 kimewaonesha waandamanaji wenye mihemuko wakivunja makazi ya Hasina yaliyopo Dhaka, na kuzipungia mikono kamera huku wakiingia enao la nyumba hiyo.

Waziri Mkuu Sheikh Hasina amejiuzulu na kuikimbia nchi kufuatia maandamano ya kumpinga ambayo yamepelekea mamia ya watu kufa.

Waandamanaji 90 wameuawa siku ya jana Jumapili katika mapambano na polisi, na kufanya idadi ya vifo kufikia watu 300 katika wiki za hivi karibuni.

Chapisha Maoni

0 Maoni