Aliyezusha binti aliyebakwa mtungo kafa akamatwa

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Amos Lutakulemberwa Lwizamiaka (54)  mkazi wa Tegeta Wazo Kinondoni kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kwamba binti aliyerekodiwa video Agosti 2024 akifanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa kubakwa na kulawitiwa amekutwa amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro ameeleza kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema anahojiwa na polisi kutokana na kutoa taarifa za uongo zenye lengo la kuzusha hali ya taharuki.

"Jeshi la Polisi linatoa wito watu kujiepusha na kutoa au kuchapisha taarifa za uongo zenye malengo ya kuzusha taharuki katika jamii kwani kufanya hivyo ni makosa lakini litaendelea kuzingatia maoni ya watu ambayo hayakinzani na sheria za nchi," amesema kamanda Muliro.

Chapisha Maoni

0 Maoni