Wananchi wa Rwanda wajitokeza kuchagua rais

 

Wapigakura Rwanda wamepanga foleni katika vituo vya kupigia kura leo Julai 5, kumchagua rais ajaye, huku rais aliyemadarakani Paul Kagame akitarajiwa kushinda.

Rais Paul Kagame mwenye umri wa miaka 66 ameliongoza taifa hilo la Afrika ya kati karibu kwa robo ya karne, na amekuwa akishinda chaguzi zilizopita kwa zaidi ya asilimia 90.

Wagombea wanane waliomba kuwania urais kumg'oa madarakani Kagame, lakini ni wagombea wawili tu waliopitishwa na tume ya uchaguzi kuwania urais.

Wagombea wengine akiwamo wakosoaji wakubwa wa Kagame, wamezuiwa kuwania uchaguzi kwa sababu mbalimbali zikiwamo za kuwa na rekodi ya uhalifu.

Chapisha Maoni

0 Maoni