Wadau waombwa kusaidia ujenzi wa Zahanati 17 Musoma Vijijini

 

Jimbo la Musoma Vijijini linahitaji michango ya wadau mbalimbali ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa Zahanati 17 ambazo zinajengwa kutumia michango ya wanavijiji na wadau wao wa maendeleo.

Jimbo hilo lenye Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374 lina Hospitali moja ya Halmashauri/Wilaya inayotoa Huduma za afya na vituo vitatu vya afya vya Kata vinavyotoa Huduma za afya.

Pia jimbo lina Zahanati zinazotoa huduma za afya za Serikali 26 na za binafsi nne pamoja na Vituo vya Afya vya Kata vitatu vinavyosubiri kufunguliwa na tayari vifaa vya matibabu vimeanza kupelekwa.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo imesema kuwa baadhi ya Zahanati zinazojengwa zimeanza kupokea fedha kutoka Serikalini.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuanza kutoa michango ya fedha kwa baadhi ya Zahanati tunazojenga, na tunatoa wito kwa wadau wakiwamo wazaliwa wa Musoma kuchangia ujenzi,” imesema taarifa hiyo.

Ujenzi wa Zahanati 17 unafanyika kwenye vijiji 17, vya Bulinga, Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege,  Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu.

Chapisha Maoni

0 Maoni