Rais Biden atangaza kujiondoa kuwania urais wa Marekani

 

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais, kufuatia ongezeko la shinikizo kutoka kwa chama cha Democratic.

Biden amesema uamuzi wake wa kujiondoa kuwania urais, “ni kwa masilahi bora ya chama chake pamoja na nchi ya Marekani”.

Rais Biden amemuidhinisha Makamu wake wa Rais Kamala Harris, kuwa mgombea mpya wa urais wa Marekani wa Democratic.

Amechukua uamuzi huo ikiwa imebakia miezi minne tu kabla ya wananchi wa Marekani kupiga kura kumchangua rais.

Biden mwenye umri wa miaka 81, amekuwa akikabiliwa na wito wa kujiondoa baada ya kuvurunda kwenye mdahalo dhidi ya mgombea wa Republican Donald Trump, mwezi Juni.

Chapisha Maoni

0 Maoni