Naibu Waziri Mambo ya Nje aandika barua ya kujiuzulu ubunge

 

Mbunge wa kuteuliwa na Rais na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk ameandika barua ya kujiuzulu Ubunge kwa Ofisi ya Spika wa Bunge.

Katika barua yake hiyo kwa Spika, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk ameeleza sababu za kufikia uamuzi huo kwa kile alichoeleza kuwa anakabiliwa na changamoto za kijamii hivyo anahitaji muda kuzishughulikia.



Chapisha Maoni

0 Maoni