Nani kuibuka mbabe Uingereza na Hispania fainali ya Euro 2024?

 

Uingereza kutoana jasho na Hispania jumapili hii kwenye Fainali ya Euro 2024 Jijini Berlin baada ya kufanikiwa kuifunga Uholazi kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali jana usiku.

England wanatarajia kupiga hatua zaidi ya ilivyokuwa Euro 2020, ambapo walipoteza mchezo wao wa fainali kwa mikwaju ya penati dhidi ya Italia.

Hata hivyo safari hii pia wanakabiliana na timu bora kwenye Euro 2024 ya Hispania ambayo imeshatwaa ubingwa wa Euro mara tatu.

Rekodi zipoje za Uingereza dhidi ya Hispania ?

Mwaka 1980 katika hatua ya makundi Uingereza iliifunga Hispania magali 2-1 huko Napels, ingawa timu zote hizo zilitolewa kwenye michuano.

Na mwaka 1996 mataifa hayo yalikutana katika hatua ya 16 bora kwenye dimba la Wembley, na Uingereza ikashinda kwa matuta, baada ya kutoka suluhu.

Katika michuano mingine ya kimataifa mwaka 1950 kwenye Kombe la Dunia, Hispania ilishinda goli moja kwa bila kwenye hatua ya makundi huko Rio de Janeiro.

Chapisha Maoni

0 Maoni