Kibu Denis katorokea Ulaya, Msimamizi wake amuombea radhi Simba SC

 

Msimamizi wa Kibu Dennis, Rashid Yazidu wa Kampuni ya Football Fraternity ameibua mapya kuhusu sakata la mshambuliaji huyo wa Simba SC ambapo amesema kuwa nyota huyo ameshawishiwa na ametoroshwa kwenda Ulaya.

“Kama mlivyoiona taarifa, klabu imekuwa confused (changanyikiwa) kuhusu wapi alipo mchezaji. Siku tatu nyuma nilikosa mawasiliano na mchekeshaji, nikawa na maswali, viongozi wananiuliza yupo wapi mchezaji?,” alisema Yazidu katika mahojiano na Radio ya Wasafi.

“Jana tumepata uhakika zaidi kuwa mchezaji yupo Ulaya. Jana ndio ameondoka airport (uwanja wa ndege) kwenda Ulaya, lakini mimi nilikuwa najua yeye yupo Kigoma kwa matatizo ya kifamilia,” aliongeza Yazidu.

Yazidu ameeleza kuwa mchezaji ameshawishiwa na ametoroshwa kwenda Ulaya, mchezaji hana ‘technical know how’ yeye ni mtaalamu wa mpira! ameshawishiwa na kufanya mipango ya kuondoka kwenda Ulaya.

“Kilichotokea ni utovu wa nidhamu kwanza yeye kwenda Kigoma kwenda kumuuguza mzazi wake hakutoa taarifa kabla baadaye mimi niliitaarifu klabu juu ya suala la matatizo yake ya kifamilia,. taarifa za kuuguliwa na mzazi alizitoa kwa kiongozi Simba ambaye sio sahihi,” alisema Yazidu.

“Mimi ndiye ninayetambulika na Simba Sc, nimeanza kumsimamia kuanzia dili lake la kwanza Simba SC, awali nilikuwa mwanasheria ya Kibu tu kabla ya Jamal (aliyekuwa wakala wake) kunikabidhi baada ya kuwa na majukumu mengine nje ya nchi,” alisema Yazidu.

Yazidu ameomba radhi kwa niaba ya mchezaji huyo kwa Simba SC, na kusema kuwa mchezaji wake hakujua athari za alichokifanya cha kuachana na Simba kwa kutorokea Ulaya, na kusema alishawishiwa na kuaminishwa na kujikuta amejiingiza kwenye matatizo.

Chapisha Maoni

0 Maoni