Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania
kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuleta mapinduzi sekta ya
Umwagiliaji, hivyo miradi yote aliyoahidi itatekelezwa.
Waziri Bashe amesisitiza utekelezaji wa miradi hiyo
unaofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji si hadithi bali umelenga kuinua
sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Ameitakata Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujipanga kuhakikisha
wanatekeleza miradi hiyo na wananchi wapuuze wanaowalaghai kuuza mashamba.
Waziri Bashe amesema hayo Wakati akizungumza na wadau wa
umwagiliaji katika eneo la mradi wa Luiche, ambapo amemshukuru Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.
“Leo tumefanya uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Umwagiliaji
katika Bonde la Luiche Wilayani Kigoma katika Mkoa wa Kigoma. Miradi hiyo yenye
thamani ya zaidi ya bilioni 60 itakwenda kunufaisha zaidi ya wakulima 9312
kupitia kilimo cha Umwagiliaji”.
Ameongeza kuwa, wizara inamshukuru Rais Dkt. Samia kwani
anafanya kwa vitendo na hataki utani katika kilimo cha umwagiliaji.
“Tunamshukuru sana
sana Rais kwa kutoa bilioni 60 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Luiche .
Msiuze aridhi yenu ambayo serikali inawekeza fedha zaidi ya bilioni 60 kwa
ajili yenu.Mkoa wa Kigoma ni Mlango wa uzalishaji na mlango wa kuhudumia nchi
jirani.Serikali inakwenda kujenga Jengo
la ghorofa tatu ambalo litakuwa kitovu cha umwagiliaji katika mkoa wa kigoma na
Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tanı 4000, Pamoja na mtambo wa
kuchakata mpunga,”alisema Waziri Bashe.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi wa Bonde la
Luiche, ambao umekuwa ukizungumzwa toka nchi ilipopata Uhuru na kwamba
uwekezaji huo mkubwa uliyofanywa na serikali unakwenda kuleta mapinduzi makubwa
kiuchumi kwa wananchi wa Kigoma.
Mndolwa pia ametumia fursa hiyo kupokea maagizo ya Waziri wa
Kilimo.
“Mradi huu ni mkubwa na utazingatia uwekaji wa miundo mbinu
muhimu kama bara bara na itazingatia Kulinda vyanzo vya maji na mazingira,” alisema
Mndolwa.
Mndolwa pia aliongeza kuwa Tume imepokea maelekezo ya
Serikali kuwa mradi ujumuishe ujenzi wa
Ghala,nyumba ya watumishi Pamoja na Ofisi ya Umwagiliaji.
Wakati akiwasilisha Taarifa ya Umwagiliaji kwa Mkoa wa
Kigoma, Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Katuta Mustang, amesema
Mkoa wa Kigoma Una eneo linalo faa kwa umwagiliaji lenye ukubwa wa Hekta
147,000 na kwamba Mkoa wa Kigoma una jumla ya skimu za umwagiliaji 59 na ni
skimu 6 pekee ndizo zilizoendelezwa.
“Mradi wa Ruiche unajumuisha ujenzi wa Skimu kwa gharama ya shilingi Bilioni 40 na ujenzi wa Bwawa lenye ukubwa wa mita za mraba 710,000 kwa gharama ya shilingi Bilioni 24,na ujenzi wa mifereji yenye urefu wa jumla ya kilomita 100 kutoa maji mashambani;ujenzi wa nyumba mbili za watumishi na usanifu wa jengo la Umwagiliaji Mkoa,” alisema Katuta.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli
emahakikishia serikali kuwa serikali itahakikisha ulinzi wa Mradi na Kumshukuru
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na waziri wa kilimo Hussein Bashe kwa
kufikisha huduma ya Umwagiliaji katika wilaya ya Kigoma.
Akimkaribisha Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto Thobias Andengenye, ameishukuru serikali
kwa uwekezaji Mkubwa unaofanywa katika Mkoa wa Kigoma, kupitia kilimo cha
umwagiliaji.
“Kilimo cha umwagiliaji ni mühimu sana katika kuinua uchumi
wa Mkoa wetu wa Kigoma kwani Mkoa wetu una zaidi ya hekta 100 zinazofaa kwa
umwagiliaji lakini mpaka sasa ni hekta 9000 tu ndizo zinazo tumika,” amesema
Andengenye.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Ngenda Shabani Kirumbe, amemshukuru
raid Dkt. Samia Suluhu Haasan kwa kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Luiche
kwani kufanya hivyo kutawezesha kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika mkoa wa
Kigoma.
“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Haasan kwa uwekezaji wa
zaidi ya Trilioni 3 katika Mkoa wetu wa
Kigoma na kutupatia Bilioni 60 za utekelezaji wa Mradi wa Umwagiliaji
Luiche.Kataeni watu wanao taka kuwarudisha nyuma kwa kuwadanganya kuwa mtapewa
fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miradi ya miundo mbinu,” alisema Ngenda.
Mradi wa Luiche upo katika wilaya ya kigoma, mkoa wa Kigoma. Mradi huu unajumuisha vijiji vya Kamara, Simbo, Kaseke, Nyamori, Msimba, Matiazo pamoja na Kagera. Mradi huu utakuwa na ya hekta 3000 zitakazomwagiliwa baada ya ujenzi kukamilika. Mradi huu wa Luiche umegawanyika katika mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa ujenzi wa bwawa pamoja na mkataba wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji.
0 Maoni