Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa wilayani Nyang'wale, Geita

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Geita, Juni 2, 2024. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua jengo la Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita, Juni 2, 2024. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa Sabasaba uliopo Karumwa wilayani Nyang’hwale, mkoa wa Geita, kuhutubia mkutano wa hadhara, Juni 2, 2024.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajasiliamali waliowezeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzindua Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililopo Karumwa wilayani Nyang’wale mkoani Geita, Juni 2, 2024. Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, Grace Kingarame. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo za batiki alipotembelea banda la maonesho la wanawake wajasiriamali waliowezeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzindua kituo cha baraza hilo kilichopo Karumwa wilayani Nyang’wale mkoa wa Geita, Juni 2, 2024.   Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng'i Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chapisha Maoni

0 Maoni