Waziri Kairuki afungua Maonesho ya Kimataifa ya Kili-Fair

  

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii maarufu kama Kili-fair leo Juni 7, 2024 Jijini, Arusha. 

Akizungumza katika Maonesho hayo Waziri Kairuki amepongeza waanzilishi wa maonesho hayo ambapo wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za utalii zaidi ya 800 wapo kwenye maonesho hayo. 

Aidha, Waziri Kairuki amewahakikishia wadau wa utalii kuwa serikali inawaunga mkono kwa asilimia 100 ili kufikia adhma ya watalii milioni tano na mapato ya dola bilioni 6 ifikapo 2025.

Vile vile, Waziri Kairuki amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kuwa moja ya wadhamini wa maonesho hayo ambayo ni chachu ya Maendeleo ya Utalii nchini.



Chapisha Maoni

0 Maoni