Jen. Mkunda awavisha nishani Maafisa na Askari kanda ya Dar na Pwani

  

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewavisha nishani Maafisa na Askari wa Vikosi vilivyoko Kanda ya Dar es Salaam na Pwani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hafla hyo imefanyika Jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Mgulani leo tarehe 7 Juni  2024 kwa kuwavisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, Nishani ya Utumishi Mrefu na Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia njema. 

Wakati huo huo, Jenerali Mkunda amewavisha Nishani ya Ulinzi wa Amani ya SADC Maafisa na Askari kwa niaba ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kwa kutambua mchango wao katika Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya Mwavuli wa SADC iliyowatunuku Nishani hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni