Rais Samia akiwa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga Korea

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni mbalimbali, Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) mara baada ya kutunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima kwenye Sekta ya Anga (Honoris Causa) na Chuo hicho Jijini Seoul Jamhuri ya Korea tarehe 03 Jun1, 2024.

Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Profesa Hee Young Hurr akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo hicho wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia Chuoni hapo Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mfanyakazi wa Ndege kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Sang bin Jeon aliyekuwa akielezea kuhusu sehemu mbalimbali za Ndege aina ya Airbus A300-600R ambayo ipo kwa ajili ya Maonesho na mafunzo kwa Wanafunzi katika Chuo hicho Jijini Seoul tarehe 03 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiangalia  sehemu mbalimbali za Ndege aina ya Airbus A300-600R ambayo ipo katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) kwa ajili ya Maonesho na mafunzo kwa Wanafunzi,  Seoul tarehe 03 Juni, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni