Gachagua amshushia zigo la maandamano Mkurugenizi wa Usalama wa Taifa

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amewatupia lawama Usalama wa Taifa (NIS), kwa kuzembea kuhusu maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha na kumtaka Rais William Ruto kumfukuza kazi Mkurugenzi wa (NIS) Noordin Haji.

Gachagua amesema Rais Ruto hakuwa na taarifa kuwa watu hawautaki Muswada wa Fedha wa 2024. "Iwapo rais angekuwa anajua watu hawautaki muswada huo asingewaomba watu wake wauidhinishe bungeni."

Tuna Idara ya Usalama wa Taifa ambayo ilipaswa kumpatia taarifa hizo rais, lakini hawakufanya hivyo, alisema Gachagua.

Gachagua ametoa kauli hiyo saa chache tu kupita tangu Rais William Ruto kukataa kutia saini muswada huo na kuurudisha bungeni ili ukafanyiwe mabadiliko yanayolalamikiwa na wananchi.

Hatua hiyo, inafuatia ghasi zilizotokea jana bungeni baada ya waandamanaji vijana kulivamia bunge kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya na kufanya uharibifu.

Kwa mujibu wa Tume ya Haki za Binadamua Kenya (KNHRC) watu wapatao 22 walifariki katika maandamano yaliyofanyika jana.

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Kenya (NIS) Noordin Haji kibarua chake kipo mashakani kufuatia maandamano ya vijana wa Gen Z ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024.


Chapisha Maoni

0 Maoni