Wanachama wa JET watembelea Makuyuni Wildlife Park

 

Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) leo April 30, 2024 wametembelea Makuyuni Wildlife Park iliyopo wilaya ya Monduli katika mkoa wa Arusha kwa lengo la kujifunza Uhifadhi wa wanyamapori na kujionea shughuli za Utalii.

Ziara hii ya mafunzo imefanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa  "Tuhifadhi Maliasili" unaoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET)  kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID).

Mojawapo ya malengo ya Mradi huu ni kuokoa shoroba za wanyamapori zilizoathirika na uvamizi wa binadamu. Na Makuyuni ikiwa ni sehemu ya ushoroba wa Ziwa Manyara/Tarangire ilikuwa ni sehemu sahihi kupatembelea.

Waandishi hao wapatao saba (7) wametokea vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Clouds TV na Redio,  magazeti ya Nipashe, Zanzibar Leo,  Daily News na The Guardian.

Aidha, katika ziara yao ndani ya Wildlife Park hiyo walipata fursa ya   kujionea wanyamapori mbalimbali kama vile twiga, pundamilia, pofu, nyati, ngiri, swala, tembo, pamoja na ndege kama vile kanga, tumbusi, njiwa na wengine wengi.




Chapisha Maoni

0 Maoni