Waziri Mkuu akagua maandalizi kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kisongo Aprili 30 2024. Kesho atashiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani- Mei Mosi ambayo kitaifa yanafanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani humo, Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri MKuu Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mei Mosi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.  Maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa mkoani humo na Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Deogratius Ndejembi  alipokagua maandalizi kuelekea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi  Duniani - Mei Mosi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha Aprili 30, 2024, Maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa mkoani humo na Mgeni Rasmi atakuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mary Maganga (kulia) na Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA),Tumaini Nyamhokya (Wapili kulia) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chapisha Maoni

0 Maoni