Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la
Kianglikana na Taasisi nyingine za dini kwa kudumisha amani na utulivu.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Kiongozi wa
Kanisa la Kianglikana Duniani, Askofu Mkuu
Justin Welby na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 11 Mei 2024.
Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Askofu Justin Welby kwa ujio
wake Zanzibar.
Naye Askofu Justin Welby amempa pole Rais Dk. Mwinyi kutokana
na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali
Hassan Mwinyi
Vilevile ujumbe huo umempongeza kwa jitihada zake za
kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi atashiriki kesho Ibada ya Maridhiano kutokana na madhila waliyofanyiwa Waafrika wakati wa Biashara ya utumwa katika Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini itakayoongozwa na Askofu Mkuu, Mhashamu Justin Welby.
0 Maoni