Dereva wa Lori aliyesababisha ajali ashikiliwa na Polisi Mbeya

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva aitwaye Said Rajab [35] mkazi wa Dar es Salaam aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.422 AKF/T.303 APW Scania Lori mali ya Amani Uledi wa Moshi baada ya kusababisha ajali iliyopelekea majeruhi watatu.

Ajali hiyo imetokea Mei 06, 2024 majira ya saa 7:30 mchana eneo la Mbembela Jijini Mbeya katika barabara kuu ya  Mbeya – Songwe wakati Gari hilo lililokuwalikitokea Dar es Salaam kuelekea Zambia likiwalimebeba mchele kuachanjia, kupindukana kugonga Pikipiki ainaya TVS ambayo namba yake yausajili bado kufahamika kutokana na kuharibika iliyokuwaikiendeshwa na Ambakisye Ruben Kyejo [41] mkazi wa Chunya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya SACP Abdi Issango amesema katika ajali hiyo watu watatu wamejeruhi wakiwemo Dereva wa Lori hilo, aliyekuwa Dereva wa Pikipiki Ambakisye Kyejo na aliyekuwa tingo wa Lori hilo Kasim Hussein [22] mkazi wa Dar es Salaam ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Kaimu Kamanda Issango ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa Gari T.422 AKF/T.303 APW Scania Lori kushindwa kulimudu gari kwenye eneo lenye mteremko mkali.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva kuwamakini hasa katika maeneo yenye milima na miteremko mikali ilikuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Chapisha Maoni

0 Maoni