Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na waliokuwa walinzi wa aliyekuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa Kumbukumbu ya miaka 40
tangu kifo chake, iliyofanyika Monduli mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.
Kulia ni aliyekuwa Mlinzi Mkuu Abihudi Michael Luila
aliyekuwa gari ya nyuma wakati ajali inatokea na kushoto Mlinzi wa zamu Yusto
Chuma ambaye alikuwa gari moja na Hayati Sokoine. Chuma wakati huo naye
alijeruhiwa vibaya sana na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 14.
Hayati Sokoine alifariki dunia tarehe 12 Aprili, 1984 kwenye ajali ya gari iliyotokea Wami Dakawa Wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
0 Maoni