Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akielekea kwenye eneo la Makaburi kwa ajili ya kuweka shada la maua
wakati wa Maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea mauaji ya Kimbari Kigali nchini
Rwanda. Maadhimisho hayo ya miaka 30 yamefanyika katika Makumbusho ya Mauaji ya
Kimbari, Kigali nchini Rwanda na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali
tarehe 07 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akitoa Heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye eneo la
Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda tarehe 07
Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka shada la maua
kwenye eneo la Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda
tarehe 07 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakimshuhudia Rais wa Rwanda Mhe.
Paul Kagame akiwasha mwenge wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali
nchini Rwanda tarehe 07 Aprili, 2024.
0 Maoni