Rais Mwinyi awakabidhi Simba Kombe la Ubingwa wa Muungano

 

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewakabidhi timu ya Simba shilingi milioni 50 ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Muungano kwa mwaka huu katika uwanja wa New Amaan Complex tarehe 27 Aprili 2024.

Katika mchezo huo uliochezwa jana usiku timu ya Simba SC imeifunga goli moja kwa sifuri timu ya Azam FC.

Mashindano hayo yamerejea tena nchini ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Miaka 20 imepita tangu kusimama kwa mashindano hayo ambayo yamemalizika kwa kushirikisha timu za Zanzibar na Tanzania Bara ikiwemo Simba, Azam, KMKM na KVZ.

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewakabidhi Simba fedha shilingi milioni 50 ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Muungano kwa mwaka huu.








Chapisha Maoni

0 Maoni