Nchimbi atoa salamu za Rais Samia akiwa njiani kuelekea Rukwa

 

Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akisalimiana na Wananchi wakazi wa Kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi akiwa njiani kuelekea Mkoani Rukwa.

Balozi Dkt. Nchimbi ametoa salamu za upendo za Mwenyekitimwa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Wananchi hao, Balozi Dkt. Nchimbi ametoa pongezi kwa wabunge wote wa Mkoa wa Katavi kwa utekelezaji wa Ilani unaendelea uliofikia kwa zaidi ya asilimia 80%.

Vilevile, ametoa shukrani kwa kazi kubwa ya kilimo wanayoifanya wananchi wa Katavi na kuwa seheu ya Mikoa inayozalisha na kusambaza chakula Nchini.

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amehaidi kuongeza msukumo kwa serikali kutoakana na kilio chao cha uhitaji wa barabara kwa kiwango cha lami.

Chapisha Maoni

0 Maoni