Muungano Bash ilivyokonga nyoyo kwenye Hifadhi ya Pande

 

Katika kunogesha Sherehe za Muungano, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imesherehekea kwa aina yake kwa kuandaa burudani kwenye Hifadhi ya Pande liliyopewa jina la Muungano Bash.

Ubunifu huu unaoongeza burudani na ndani ya Hifadhi ya Pande katika kuendeleza kuvutia utalii, ulikonga nyoyo za watu waliohudhuria akiwemo mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko, pamoja na watu 100 walihudhuria tukio hilo la kitalii lililofanyika Aprili 26, 2024

Hifadhi ya Pande ni mojawapo ya maeneo yenye mvuto mkubwa kwa watalii na inajulikana kama "mapafu" ya Jiji Dar es Salaam kwa kuwa na mandhari nzuri iliyofunikwa na msitu wa asili wenye kutoa  hewa safi, upepo mwanana na kivuli cha kutosha nyakati za mchana.

TAWA inaendelea kuwaalika Watanzania wote hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani kutembelea na kutalii katika hifadhi hii ya kipekee.



Chapisha Maoni

0 Maoni