Makonda kafanyekazi kuusaidia mkoa wa Arusha- Rais Samia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda leo Aprili 4, 2024 Ikulu, Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 

Makonda ameapishwa pamoja na viongozi mbalimbali aliyewateua Mhe. Rais Samia, wakiwamo Waziri, Manaibua Waziri, Manaibu na Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam.

"Makonda,umefanya kazi nzuri sana kwenye chama,kilikuwa kimelala umeiamsha sasa watu wanatoka na kujua wajibu wao,umekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ulifanya kazi nzuri sana, nimekupeleka Arusha nina imani kubwa na wewe na unajua kwa nini nimekupeleka pale, kafanye kazi kuusaidia mkoa wa Arusha, kama unavyojua ni mkoa wa utalii," alisema Rais Samia.

Chapisha Maoni

0 Maoni