Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limezindua kampeni
mahususi ya kupigia kura vivutio vyake viwili ambavyo ni Hifadhi ya Taifa
Serengeti na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro ambavyo vinashindanishwa kama vivutio
bora zaidi barani Afrika, Kampeni inayoenda kwa jina la VOTE NOW”.
Akizungumza na vyombo
vya Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo “VOTE NOW” Kamishna Msaidizi wa
Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara July Beda Lyimo alisema,
“ Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
zimechaguliwa na Taasisi maarufu duniani ya World Travel Awards ikishindana na
Hifadhi shindani kutoka Botswana, Namibia, Uganda, Afrika Kusini na Kenya, kwa
upande wa Serengeti inashindana kama Hifadhi Bora Barani Afrika “Africa’s
Leading National Park 2024” na kwa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro inashindana
kama Kivutio Bora Afrika “Africa’s Leading Attraction 2024”.
Maeneo haya yamekuwa utambulisho wa Nchi ya Tanzania katika
masuala ya Uhifadhi na Utalii kupitia Filamu ya "The Royal Tour"
ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
alizitangaza Hifadhi za Taifa Serengeti na Kilimanjaro na kuiweka Nchi yetu
katika Uso wa Dunia katika masuala ya Uhifadhi na Utalii ambapo kama Taifa
tumeshuhudia matokeo chanya ya juhudi hizi za Mhe. Rais wetu.
“Tumekuja kwa watanzania wote, wadau wa utalii kuwaomba
tupige kura kwa wingi ili hifadhi hizi ziwe kidedea na kuaminika kutokana na
sifa za kipekee zilizojaliwa. Ushindi huo utaongeza idadi ya watalii, mapato
kwa taifa na kuongeza ajira kwa watanzania” aliongeza Kamishna Lyimo.
Aidha, Kamishna Lyimo alisema kuwa, kuzipigia kura hifadhi
hizi kuna faida kubwa kwa Taifa letu na vivutio vyake kwani vitaendelea
kufahamika zaidi duniani na wageni wataendelea kuja kuvitazama kwa wingi zaidi
na tutaogeza idadi ya mapoto kama
ambavyo ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotuelekeza kufikia watalii million
tano na mapato ya dolla billioni sita
ifikapo mwaka 2025.
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo hiyo ya Hifadhi
Bora Barani Afrika kwa mara tano mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2023
ambapo kwa kura yako mwaka huu 2024 itaiwezesha Hifadhi hii kushinda kwa mara
ya sita mfululizo huku Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro imeshinda tuzo ya kivutio
Bora Barani Afrika mwaka 2013, 2015, 2016, 2017, na 2018 ambapo kwa kura yako
tutaleta ushindi huu nyumbani kwa mara ya sita. Ili kupiga kura zako tembelea
tovuti ya www.worldtravelawards/vote.
Na. Edmund Salaho/Arusha
0 Maoni