Wakamatwa wakitorosha dhahabu ya sh bilioni 1.5

 

Kamanda wa Polisi wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga akiwa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakionyesha dhahabu iliyokamatwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na kikosi kazi cha madini cha taifa linawashikilia watuhumiwa kumi wote wakazi wa Ilomba Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusafirisha na kutorosha vipande vya madini aina ya dhahabu.

Kamanda wa Polisi wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga, amesema watuhumiwa walikamatwa Machi 16, 2024 huko maeneo ya VETAIkulu, Jijini Mbeya wakiwa na vipande 314 vya madini aina ya dhahabu vyenye uzito wa gramu 9,622.76 sawa na thamani ya shilingi 1,515,621,987.03bila kuwa na kibali cha kusafirisha madini hayo.

Pia, amasema watuhumiwa walikutwa na vifaa vingine ambavyo ni vipimo vya dhahabu, majiko, mitungi ya gesi na kasiki ya kuhifadhi fedha. Watuhumiwa wamekuwa wakitorosha madini hayo kupitia njia zisizo rasmi kwa lengo la kukwepa kulipia kodi, ushuru na gharama nyingine zinazohitaji kwa wafanyabiashara ya madini.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wafanyabiashara ya madini kufuata taratibu ikiwa ni Pamoja na kukata vibali vya kufanya biashara hiyo na kulipa gharama zinazohitajika ili kuepuka usumbufu na hasara pindi wanapobainika kufanya biashara bila kufuata utaratibu.

Chapisha Maoni

0 Maoni