Upendo ndio nguzo ya viongozi wa CCM Chalinze- Ridhiwani

 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema upendo ndio nguzo ya mafanikio ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Halmashauri ya Chalinze.

Mhe. Ridhiwani ametoa kauli hiyo alipokuwa anaongea na viongozi wa CCM wa Halmashauri ya Chalinze alipowaalika kwenye Futari aliowaandalia nyumbani kwake Msoga, wilayani Chalinze mkoani Pwani.

Futari hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha CCM wilayani hapo akiwepo Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndg. Abdul Sharif Zahor na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya kutoka kata zote za Jimbo la Chalinze.

Mhe. Ridhiwani aliandaa Fuatari hiyo ili kuwakutanisha viongozi wa wilaya ya Chalinze ikiwa ni pamoja na kuupokea mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kuwaombea na kuwarehemu viongozi waliowahi kuongoza wilaya hiyo na amani ya wilaya hiyo na wazee.


Chapisha Maoni

0 Maoni